Maporomoko ya ardhi yasababisha vifo vya watu 13 marekani

Watu 13 wamefariki dunia kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kusini mwa jimbo la California, Marekani.

 

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yameathiri baadhi ya maeneo ambayo yaliathiriwa na moto mkubwa wa nyika na yameharibu barabara kuu ya pwani umbali wa maili 30 (48km).

Mawe makubwa yalimeguka kutoka milimani na kuziba barabara

Wengine 163 wamelazwa hospitali, 20 wakiwa na majeraha yanayohusiana na mvua kubwa.

Maafisa wa uokoaji wamesema kuna watu kadhaa ambao hawajulikani waliko na kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda.

Maafisa wa Kikosi cha Ulinzi Baharini wametuma ndege kadha kusaidia juhudi za uokoaji na wametahadharisha umma dhidi ya kutumia ndege zisizo na marubani kwani zitatatiza juhudi za uokoaji.

Maelfu ya wakazi wa California waliamrishwa kuondoka makwao Jumatatu, mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili. Mara ya kwanza ilikuwa ni kwa sababu ya moto, wakati huu ni kwa sababu ya mvua.