Naibu Waziri Mohammed Ahmada awaondoa hofu wanakijiji cha Mgonjoni Unguja
Naibu Waziri wa Ujenzi,Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Mohammed Ahmada amesema Wizara yake haijasahau agizo la Rais wa Zanzibar la kutengenezwa barabara kwa kiwango cha fusi kijiji cha mgonjoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Akizungumza na Zanzibar24 amesema kufuatia malalamiko ya wananchi wa eneo la kijiji hicho kuhitaji huduma muhimu za maendeleo ikiwemo barabara,kituo cha afya,Maji na umeme Serikali tayari imesha tekeleza ahadi hizo ambapo sasa ujezi wa barabara umekwama kutokana na kuharibika kwa baadhi ya vifaa na mashine kumuhimu za kusambazia kifusi na kuwataka wananchi hao kuwa na uvumilivu kwani serikali ipo mbioni.
Ahmada amesema licha ya kuharibika kwa vifaa hivyo lakini pia ujenzi ulisitishwa pia kutokana na mvua za vuli zilizokuwa zikinyesha hadi pale zitakapobungu na kuahidi ndani ya kipindi hichi baada ya kumalizika kwa sherehe za mapinduzi ya Zanzibar barabara hiyo itajengwa ili kuwaondelea usumbufu wananchi wa kijiji hicho pamoja na wapiti njia.
Aidha amesema kumalizika kwa barabara hiyo kutaweza kuwarahisishia wananchi katika kupata maendeleo na upatikanaji wa usafiri wa uhakika pamoja na kupunguza kasi ya umaskini kwani njiani hiyo itatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kujitafutia riski zao.
Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohammed Shein alitoa agizo kwa Wizara ya ujenzi kuwajengea barabara wananchi wa mgonjoni pamoja na huduma zote muhimu wapelekewe.
Amina Omar