Ngozi ya mrembo Kendall Jenner yazua gumzo

Ngozi ya mrembo Kendall Jenner, kutoka familia ya Kardashian imezua gumzo mtandaoni baada ya kuonekana kuwa na vipele vikubwa  usoni huku  shingo yake ikionekana ya kizee.

Picha zilizopigwa katika usiku wa tuzo hizo za Golden Globes  zilizofanyika mapema wiki mrembo  mwenye miaka 22 ambaye alitinga gauni jeusi kuashiria hali ya Amani zilioneshwa na kituo cha E! kuonyesha hali yake ilivyo kwa sasa.

Baada ya muda mchache baadhi ya watu walimdhihaki  mrembo huyo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kuandika “Ok but @KendallJenner showing up and strutting her acne while looking like a gorgeous star is what every girl needs to understand.” Naye Kendall akamjibu kwa kuandika “Never let that sh** stop you!”