Picha: Wananchi wakesha wakinywa uji kutii agizo la mtoto wa maajabu

Wakazi wa maeneo mbalimbali mkoani Mtwara na maeneo jirani wamejikuta wakikesha nje ya nyumba zao usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2018, wakipika na kunywa uji utokanao na unga wa muhogo. 

Wananchi hao wamedai kuwa wanatekeleza agizo la mtoto mdogo aliyezaliwa katika kijiji cha Mchichira kilicho kati ya nchi ya Msumbiji na mkoa wa Mtwara na kisha papo hapo kuanza kuzungumza kwa kutoa agizo kwa wananchi wa Mtwara.

Imeelezwa kuwa mtoto huyo alisema kuwa mvua ya maajabu yenye sumu itanyesha katika maeneo hayo na ili kujikinga nayo, watu wanapaswa kunywa uji huo kwa Imani kuwa uji huo utazuia kabisa mvua hiyo ya ajabu.

Kutokana na agizo hilo usiku wa jana watu waliendelea kuamshana nyumba hadi nyumba na wengine kupigiana simu usiku wa manane ili kunywa uji huo.

Chanzo:Azam TV