Wakili Peter Kibatala ajitoa kesi ya Wema Sepetu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Januari 10, 2018 imeahirishwa kesi inayomkabili Malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu,  mpaka tarehe 8, Februali mwaka huu.

Mahakama imepokea barua mbili kutoka kwa Wakili wa Wema, Peter Kibatala barua ya kujitoa kuwa Wakili wa Wema na nyingine kutoka kwa Wakili Alberto Msando ya kuwa Wakili mpya wa Wema sepetu.

Wema anakabiliwa na kesi ya kukutwa na misoko ya bangi nyumbani kwake.