RC ayoub aeleza utaratibu kwa watu watakaoingia katika maadhimisho ya miaka 54 ya mapinduzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhammed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kuazimishwa januari 12 mwaka huu.

Akitowa taarifa kwa vyombo vya Habari kuhusiana na Maadhiumisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Muhammed Mahmoud amesema Serikali kupitia vikosi vya ulinzi na Usalama watahakikisha maadhimisho hayo ayanafanyika katika hali ya amani na usalama.

Amesema Maadhimisho hayo yatahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serika ya Tanzania Bara.

Amesema miongoni mwa Viongozi watakaohudhuria katika maadhimisho hayo ni pamoja na Rais wastaafu, Makamo wa Rais Wastaafu na Mawaziri Wakuu wastaafu.

 Akizungumzia Utaratibu wa Watu watakaoingia katika Maadhimisho hayo amesema Washiriki wa Maandamano watakaa katika jukwaaa la Upande wa Mashariki ambapo jukwaaa la Upande wa Magharibi watakaa Viongozi na Wageni waalikwa.

Aidha amesema watu ambao hawatashiriki maandamano ya maadhimisho hayo watalazimika kukaa upende wa Mashariki (Jukwaa la saa) na Jukwaa la Kaskazini.

 Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yameanza na Shamrashamra za ufunguzi wa miradi kumi na nane ya maendeleo unguja na pemba ambapo miradi 13 imezinduliwa na 5 imeekewe jiwe la msingi.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.