Makamu wa Rais Samia: Serikali itaendelea kuthamini juhudi za vijana

Makamu wa Rais Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuthamini juhudi  wanazozitoa vijana katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa  taifa kwani endapo kundi hilo litaachwa nyuma itaweza kubadilisha mustakabali wa taifa katika kipindi kifupi.

Akizungumza katika Uzinduzi wa baraza la vijana Zanzibar katika ukumbi wa baraza la wawakilishi la zamani amesema vijana wanamchango mkubwa katika harakati mbalimbali za kuleta maendeleo nchni hivyo ameahidi kuyaunga mkono na kuyaendeleza mabaraza ya vijana Zanzibar na bara.

Hata hivyo Samia amesema uwepo wa mabaraza  ya vijana nchni imesaidia kuwainua vijana na kujitambua  kwani wananafasi kubwa katika kujiendeleza kiuchumi  kupitia mabaraza hayo na kuondokana na tatizo la ajira  na kuwataka wasome kwa bidii teknolojia kwani  ujio wa viwanda Tanzania utaweza kuwakomboa.

Akizungumzia suala la mitandano ya kijamii amewataka  vijana katika baraza hilo kutumia vizuri  mitandao kwa ajili ya shughuli zao za kupashana habari kwani itasaidia  kulijenga baraza lao pamoja na kujitangaza ili mataifa mbalimbali waweze kulitambua.

Amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018  serikali imetenga jumla ya Shilling Million mia moja kwa ajili ya mabaraza ya vijana Zanzibar ili kutekeleza shughuli zao mbalimbali na kimaendeleo.

Amina Omar