Tunisia waeka maandamano kupinga mfumuko wa bei za mahitaji muhimu

Polisi wamekuwa wakirusha mabomu ya machozi kwa kundi kubwa la watu ambao wamekuwa wakilalamikia juu ya mfumuko wa bei ambao unaathiri upatikanaji wa mahitaji muhimu.

Muendelezo wa siku tatu wa ghasia za maandamano nchini Tunisia katika mji mkuu wa Tunis na miji mingine ya nchi hiyo.

Waziri mkuu , Youssef Chahed amelaani kwa kile alichokiita kuwa ni hakikubaliki kwa kuwepo kwa fujo za waandamanaji.

Wafanyabiashara wengi wamekamatwa na polisi na kuibiwa huku vyombo vya usalama wakiwa wamewekea mkazo kulinda majengo ya serikali.

Watu wapatao mia mbili wamefungwa mpaka sasa na huku kuna mpango mwingine wa kuwepo kwa maandamano mengine makubwa hapo kesho.