IGP simon sirro awataka askari wa FFU kuwa na nidhamu

Mkuu wa Jeshi la Polisi  Tanzania IGP Simon Sirro amekitaka kikosi cha kutuliza ghasia FFU  kanda  ya Zanzibar kuwa na nidhamu ya kazi hasa  katika kulinda mali na fedha za jeshi zinazopatikana  kuzitumia kwa malengo.

Akizungumza na Askari  wa FFU wa Mikoa mitatu  katika ziara yake aliyoifanya Zanzibar amesema kikosi cha kutuliza ghasia kina kazi kubwa katika mapambano mbalimbali nchini hivyo ni vyema  kujipanga na kuongeza kasi ya mapambano ili kukabiliana na matukio yanayotokea.

Amesema  kikosi hicho bado kina kabiliwa na matatizo mengi ikiwemo ufinyu wa vitendea kazi na kuwaahidi kuwapatia magari matano makubwa  ya kufanyia kazi pamoja na gari ndogo la kusaidia katika kituo cha afya.

IGP sirro  baada ya mazungumzo na askari hao pia alitembelea  kambi za askari wa mikoa mitatu Zanzibar pamoja kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa kambi ya kikosi cha  FFU huko matemwe.

Amina Omar