Majina ya wafugwa 12 wa Pemba na Unguja walio waliopata msamaha wa Rais

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi ametoa msamaha kwa wafungwa  kumi na mbili ambao walikuwa wakitumikia  vyuo cha mafunzo unguja na pemba kwa makosa mbalimbali.

Kwamuji wa taarifa iliyotolewa na katibu wa baraza la Mapinduzi na katibu mkuu kiongozi Dr. Abdulhamid Yahya Mzee amesema Rais wa Zanzibar anaamuru  na kueleza  kuwa kifungo kilichobaki  cha wanafunzi walionufaika na msamaha  huo, ambao bado wanaendelea kutumikia  katika vyuo  vya mafunzo kwa kipindi  hichi chote  kinafutwa na wanafunzi hao watakuwa huru.

Hatua hiyo imefuatia kutokana Zanzibar  itakuwa  inasherehekea  miaka 54 ya mapinduzi  hapo  ifikapo tarehe 12 januari 2018 na Dr.Shein ameridhia  kuwachiwa huru wafugwa hao .

Miongoni mwa walionufaika na  msahama wa rais kwa upande wa unguja ni

Nassor Abeid Issa

Mussa Ali Vuai,

Omar Abdalla Nuhu,

Edward Jeremia Magaja

Na kwa upande wa pemba ni

Mtumwa Khamis Kaimu,

Said Seif Omar,

Masoud Seif Nassor na Seleiman Abdalla Amir.

Kwamujibu wa kifungu cha 59 cha katiba ya Zanzibar Rais anamamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa.

Amina Omar