Mbunge wa CHADEMA anena maneno makali kuwatoa hofu wapiga kura wake

Mbunge wa Jimbo la Mbozi mkoani Songwe kupitia CHADEMA, Paschal Haonga amesema hana mpango na wala hayuko tayari kuhama chama hicho na endapo ikatokea akahama, wananchi wachome moto nyumba yake anayoishi na familia yake.

Mbunge wa Jimbo la Mbozi mkoani Songwe kupitia CHADEMA, Paschal Haonga

Haonga ametoa kauli wakati akizungumza na wapiga kura wake katika mwendelezo wa mikutano yake jimboni humo.

Ametoa msimamo huo ikiwa ni njia ya kuwatoa hofu wapigakura wake baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa mbunge huyo naye ni miongoni mwa wabunge wanaohisiwa kuendelea kukihama chama hicho.

Kauli ya Haonga imekuja wakati wimbi kubwa la viongozi wa CHADEMA wakiendelea kumtimkia CCM kwa kile wananchoeleza kuwa, wanakwenda kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Pombe Magufuli.