Afariki baada ya kutolewa mimba Pemba

Mwanamke mmoja mkaazi wa Kipangani chini Wete mkoa wa kaskazini Pemba anadaiwa kufariki dunia baada ya kutoa ujauzito ambao mpaka anafariki haujajuulikana hasa ni wa muda gani ingawa mwenyewe alitamka kuwa
ni wa mwezi mmoja na nusu au miwili.

Mwanamke huyo mwenye miaka 27 ambae hakuwahi kuolewa, muda mfupi kabla ya kufariki dunia aliwaeleza madaktari wa hospitali ya wete kuwa alitolewa mimba hiyo katika nyumba moja eneo la selemu wete , mwanaume mmoja na mwanamke mmoja ndio waliyomtoa, pia aliwaeleza mtu aliyempa ujauzito huo na mengineyo.

Madaktari wameeleza kuwa Ghafla wakati anapatiwa matibabu alifariki  dunia ambapo walimfanyia upasuaji na kumtoa baadhi ya mabaki ya mtoto yaliyosalia
tumboni mwake.

Habari kamili itakujia mda mfupi.

RAUHIYA MUSSA SHAABAN.