Sugu, Emmanuel Masonga warudishwa rumande

Mbunge wa Mbeya mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’  na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyassa, Emmanuel Masonga leo Ijumaa Januari 19, 2018 wamerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana ya kesi inayowakabili ya maneno ya uchochezi hadi Januari 22, 2018 ambapo kesi yao itaanza kusomwa mfululizo. .

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya amesema sababu ya kumnyima dhamana mshtakiwa Sugu na mwenzake ni hofu ya mshtakiwa kutohudhuria mahakamani hapo mara kwa mara.

Sugu na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa wanashikiliwa na jeshi la polisi tangu Januari 16, 2018 wakituhumiwa kutenda kosa la uchochezi katika mkutano wao wa hadhara ambao ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya ambapo jeshi la polisi linasema kuwa viongozi hao walizungumza maneno yenye kuleta chuki kati ya Serikali na wananchi.