Tamasha la 15 la  Sauti za busara linatarajiwa kuanza leo tarehe 8  visiwani Zanzibar 

Tamasha la 15 la  Sauti za busara linatarajiwa kuanza leo tarehe 8  visiwani Zanzibar  katika eneo la ngome kongwe  ambalo linatarajiwa kuanza na  maonesho  10  katika majukwaa matatu tofauti.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa tamasha hilo la sauti za  busara Yussuf Mahmoud amesema kufanyika tamasha hilo kila mwaka  lengo  lake  kuu  ni kuwaunganisha  watu pamoja  wenye mila na tamaduni tofauti za kiafrika  kwa kutoa kipaumbe  kwa wasanii  wenye vipaji ambao wanacheza muziki   wenye utambulisho wa kitamaduni na kuweza kunufaika na kipaji chao.

Mkurugenzi wa Tamasha la Suati za Busara, Yusuf Mahmoud

Amesema  ili kuinua  vipaji vya wasanii wa ndani ya nchi katika tamasha hilo litaweza kuwakutanisha wasanii wa ndani na nje ya nchi kuweza kubadilishana mawazo na uzowefu wa kuwaza kufanya kazi zao kwa mashirikiano  ili kuinua tasnia ya muziki nchini.

Aidha  Yussuf amesema  tamasha  limeweza kufanikiwa kwa hatua kubwa kuitangaza Zanzibar na Tanzania  sehemu mbalimbali duniani na limeweza kuvutia  vyombo vya habari vya kimataifa  na  mapromota  wa matamsha  mbalimbali ya kimataifa  ambapo amesema  pia tamasha    litaweza kutoa fursa   kwa wasanii wa kanda ya Afrika Mashariki  kutangaza muziki duniani.

Hata hivyo amesema  mbali na  tamasha hilo kutoa fursa kwa wasanii hasa wandani  kujitangaza kupitia  sauti za busara lakini pia  fursa za ajira kutolewa  kwa vijana  hivyo ametoa wito kwa vijana kuweza kuchangamkia  fursa hizo ili kuweza kujikwamua na hali ya umaskini na kujipatia kipato.

Wakati huo huo amesema  usiku wa ufunguzi wa tamasha  kutakuwa na burudani kutoka  kwa simangavole kutoka Reunion,CAC fusion  kutoka Tanzania,Matona culture band,Zanzibar  taarab  ensemble na mauled ya  homu  ya mtendeni kutoka Zanzibar,DDC mlimani Park Orchestra,Diana Samkange kutoka Zimbabwe na kidum  kutoka  Burundi.

Wananchi wameombwa kujitokeza katika kutoa ushirikiano wao katika tamasha hilo  ili kuweza kuona  mambo mbalimbali ikiwemo  ngoma za utamaduni  na vipaji  vya  wasanii.

Miongoni mwa  wafadhili waliofafili Tamasha la sauti za busara  ni Ubalozi wa Norway,Ubalozi wa uswisi nchini Tanzania  na Zambia,Africalia,Mozeti,zanlink,Zenji fm,Chuchu fm,Tiff tv,Music in Afrika  na Ubalozi wa ujerumani na wengine,ambapo litahudhuriwa na watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.

Amina Omar