Diamond Platnumz afika mahakama ya Kisutu

Msanii wa Muziki wa Bongo Flava, Diamond Platnumz amewasili Mahakama ya Kisutu leo kwa ajili ya kusikiliza shauri linalohusu matunzo ya mtoto aliyezaa na Hamisa Mobetto.

Katika kesi ya msingi, Mobetto alimfikisha Diamond katika mahakama hiyo kitengo cha watoto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.

Mwezi Oktoba 2017 Diamond alipewa wito wa kwenda mahakani uliowasilishwa kwake na mawakili wa Mobeto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.

Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.