Kesi ya Wema Sepetu kurindima tena February 26, mwaka huu.

Muigizaji wa filamu bongo Wema Sepetu amewasili Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili ya kutumia dawa za kulevya.

Shahidi wa upande wa mashtaka Inspekta Willy ametoa ushahidi wa sampuli ya mkojo wa Wema alioupeleka kwa mkemia mkuu wa serikali kufanyiwa vipimo zaidi ambapo awali ushahidi huo ulikataliwa mahakamani hapo na aliyekuwa wakili wa Wema wa kujitolea, Mhe. Tundu Lissu.

Mahakama imeiahirisha kesi hiyo mpaka February 26, mwaka huu.