Mwanamke adai mumewe amuibia figo ili kujilipa mahari

Mwanamke mmoja nchini India amedai kuwa mumewe na nduguye wa kambo wamekamatwa baada ya kuwaambia maafisa wa polisi walimuibia figo moja ili kujilipia mahari.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba mume wa mwanamke huyo kutoka Magharibi mwa Bengal alipanga kumfanyia upasuaji wakati mkewe alipokuwa akiugua tumbo.

Baadaye mwaka 2017, alifanyiwa vipimo viwili vya ukaguzi wa kimatibabu ambavyo vilibani kwamba figo yake moja haipo.

Anadai kwamba mumewe mara kwa mara alitaka kulipwa mahari yake .

Malipo ya mahari ya aina hiyo ambayo hulipwa familia ya mume kutoka kwa familia ya mke nchini India yamepigwa marufuku nchini India tangu 1961.

Akizungumza na vyombo vya habari nchini India, mwanake huyo Rita Sarkar , alisema amekuwa na mgogoro wa kila siku nyumbani kwake kuhusu mahari hayo kwa miaka mingi.

”Mume wangu alinipeleka katika hospitali ya kibinafsi mjini Kolkata, ambapo yeye na maafisa wa matibabu waliniambia kwamba nitapona nitakapotolewa eneo hilo la utumbo lililovimba kupitia upasuaji” , gazeti la Hindustan lilimnukuu akisema.

”Mumewe wangu alinionya kutozungumza kuhusu upasuaji huo kwa mtu yeyote mjini Kolkata”

Miezi kadhaa baadaye mwanamke huyo alikuwa akihisi vibaya na akapelekwa hospitalini na watu wa familia yake.

Uchunguzi ulibaini kwamba figo yake ya upande wa kulia ilikuwa imetolewa, alisema.

Ukaguzi wa pili wa kimatibabu ulithibitisha ukweli huo.

”Baadaye nilijiuliza ni kwa nini mume wangu alinitaka kunyamazia upasuaji niliofanyiwa’, aliambia gazeti la Hindustan Times.

”Aliuza figo yangu kwa sababu familia yangu haikuweza kumlipa mahari yake”.