SMZ yapiga hatua kubwa ya kimaendeleo nchini

Mshauri wa Rais Pemba Dr. Mauwa  Abeid Daftari amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imepiga hatuwa kubwa ya kimaendeleo kwa kuwapelekea wananchi huduma muhimu katika nyanja tofauti, nakuwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali yao.

Amesema SMZ imejipanga kuwapatia wananchi huduma za lazima kamavile afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara na umeme hadi kwenye Visiwa ili kuwaondolea shida wananchi wake.

Akizungumza na Waandishi wa vyombo mbali mbali vya  habari huko katika Habarimaelezo Pemba  Dr Mauwa amesema kuwa juhudi zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar  Dr. Ali Mohd Shein niutekelezaji wa ilani ya CCM katika kuwaletea huduma za lazima wananchi wake.

Amefahamisha kuwa pamoja na SMZ kujenga Vituo vingi vya Afya katika maeneo mbali mbali lakinipia imejipanga kusaidia upatikanaji wa madawa katika vituo vyake ili kusaidia kunyanyua Afya ya Mama na Mtoto.

Mapema  Dr. Mauwa amewaelezea Waandishi hao kuwa vyombo vya habari vinawajibu mkubwa wa kuyatangaza maendeleo yaliofikiwa na Serikali ambayo yanaonekana wazi wazi ili wananchi waendelee kuiunga mkono serikali yao.