Majaji na Mahakimu watakiwa kuendesha kesi kwa haraka ili wananchi wanufaike na haki zao

Makamo wa pili wa Raisi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka majaji na Mahakimu kuendesha kesi kwa haraka ili wananchi wanufaike na haki zao za msingi juu ya mashtaka wanayoyafungua.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Shamrashamra za Siku ya sheria katika Viwanja vya Misara Mjini Unguja Balozi Seif amesema wananchi wamekuwa wakilalalmika juu ya kucheweshwa kesi.

Amesema kuharakisha kesi kutawewazesha wananchi kuwa na ari ya kuripoti kesi zinazojitokeza katika jamii ili kuzuia wimbi la wavunjifu wa sheria.

Hata hivyo balozi seif amewataka wananchi kutumia vyema fursa  ya maonesho hayo katika kujifunza sheria pamoja na kupeleka malalamiko yao kwa kwa mawakili mbalimbali waliopo ili waweze kutatuliwa matatizo ya kesi zao.

Amesema kuna wimbi kubwa la wananchi hawajui sheria jambo ambalo linasababisha kushindwa kukata rufaa baada ya kutoridhika na hukumu inayotolewa na mahakama juu ya mashtaka wanayofungu jambo ambalo linapelekea kukosa haki zao pamoja na kulalamika mitaani.

Aidha balozi iddi ametowa wito kwa Mahakama kuwa na utamaduni wa Kufungua maonesho hayo kila mwaka ili kuwawezesha wananchi kujifunza sheria za nchi yao.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othaman Makungu amesema lengo la kuwepo kwa Maonesho hayo kutowa elimu ya sheria kwa wananchi ili kujua haki zao na namna ya kufuatilia mashtaka yao mahakamani.

Amesema katika kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa Maonesho hayo pia yameshirikisha wafanya biashara mbali mbali kujifunza elimu ya sheria pamoja na kuuza na kutanga bidhaa zao hali hiyo inaenda sambamba na kauli mbinu ya siku ya sheria inayolenga kuimarisha Utawala wa sheria katika  kukuza Uchumi wa Nchi.

Siku ya sheria inatarajiwa kuazimishwa ifikapo Feb 12 ambapo kwa Zanzibar maadhimish hayo yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Barza la wawakilishi la zamani Mjini Unguja.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.