Idadi ya watu Zanzibar yaongezeka

Utafiti uliofanywa  na Serikali imeonekana Zanzibar inaongoza kwa idadi kubwa ya watu kwa afrika  ya Mashariki na kufikia Millioni Moja na nusu ikifuatiwa na Kenya.

Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabiti kombo alisikika akisema  kuwa Zanzibar kila  mwaka  zaidi ya watu Hamsini elfu wanazalikwa, na kwa siku Katika hospitali ya Mnazi Mmoja wanazaliwa watoto mia moja na katika hospitali ya Kivunge  zaidi ya mia nne kwa mwezi wanazaliwa watoto na kwaupande wa Hospitali ya Makunduchi  mia moja na 38 kwa mwezi wanazaliwa jambo linaloleta faraja kubwa nchini.

Hata hivyo Mahmoud kombo amesema licha ya jamii kuzaa sana lakini serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejipanga vyema katika kuboresha huduma za mama na mtoto kuhakikisha wanapata mahitaji yao bila ya usumbufu wowote.

Kwaupande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohammed Shein amesema  kiwango cha idadi ya watu Zanzibar kinaongezeka na kufikia Asilimia 2.8 kwa mwaka na kupelekea baadhi ya vitu kutotosheleza kutokana na idadi kubwa ya watu.

Amesema wakati wa Mapinduzi Zanzibar 1964 yanafanyika Zanzibar ilikuwa na watu  laki tatu na Ishirini  elfu lakini  hivi sasa  baada ya miaka 54  kiwango kinaongezeka na kufikia  Millioni  Moja na nusu ambapo kiwango kimeongezeka mara tano licha ya kuwa Zanzibar ni ile ile lakini watu wake wameongezeka.

Aidha Dr.Shein amesema kuongezeka kwa idadi ya watu pia kuna hangamoto  ikiwemo  kuongezeka kwa mahitaji ya jamii  kama vile skuli,vituo vya afya na mambo mengine.

 Amina Omar