Mwalimu Kilombero adai kuchagawa kwa wanafunzi ndio sababu ya kufeli mitihani

Walimu  Skuli ya Kilombero  Wilaya ya kaskazini B Unguja, wamesema kuumwa kwa wanafunzi ikiwemo kupandisha mashetani ni  miongoni mwa sababu iliyochangia wanafunzi kutofanya vizuri katika mitihani yao ya taifa ya mwaka jana 2017.

Mmoja miongoni mwa Walimu katika skuli hiyo Shaka Hassan Ali akizungumza na Zanzibar24 sababu za kufeli sana kwa wanafunzi amesema kuwa wanafunzi huchagawa mashetani  karibu na kipindi cha kufanya mitihani hali inayowakosesha amani ya kusoma vizuri na kupelekea kutojiamini kwenye mitihani na kufeli.

Amesema wamejitahidi kuwasaidia kuondokana na hali hiyo katika kipindi cha mitihani ikiwemo kutafuta masheikhe  kusoma dua katika mazingira ya skuli lakini  pia inashindikana  kuondoa tatizo hilo la mashetani katika skuli hiyo ya kilombero.

Aidha amesema huwashirikisha wazazi kuondoa tatizo hilo lakini baadhi ya wazazi  hushindwa kutoa ushirikiano  kwa walimu  hali inayopelekea sasa wanafunzi kushindwa kusoma na kufeli katika masomo yao kwani muda mwingi wanakuwa wanaumwa.

Mwalimu shaka amesema kutokana na tatizo hilo kuwa la muda mrefu na ni miongoni mwa  chanzo cha kufeli  wanafunzi hao  kwa kiwango kikubwa hivyo amezitaka mamlaka  husika kwa kushirikiana na wazazi pamoja na walimu  kushikamana ili kuwasaidia watoto hao.

Amina Omar