Sheria mpya ya kupambana na udhalilishaji itasaidia kuondosha matatizo nchini

Wasaidizi Wakuu wa Dawati la kijinsia za Polisi Zanzibar Muembe madema wamesema uwepo wa sheria mpya ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji itaweza kusaidia kuondosha matatizo katika jamii.

Wakizungumza na Zanzibar24 Wasaidizi Wakuu wa Dawati hilo wamesema vitendo vya udhalilishaji ikiwemo vya liwati,ubakaji vilivyokithiri vitaondoka endapo sheria hiyo itafanya kazi bila ya kumuonea mtu muhali ambapo kutaweza kupatikana  hukumu stahiki kwa watenda vitendo hivyo.

Wamesema sheria hiyo itaweza kuwatia hatiani  watuhumiwa wa  vitendo vya udhalilishaji ,kwani  bado kuna malalamiko kwa wananchi kuwa vifungo wanavyopewa wafanya vitendo hivyo ni miaka kidogo ukilinganisha na kosa wanalolitenda na kusema kuwa uwepo wa sheria hiyo ya kupambana na udhalilishaji Zanzibar itaweza kuwafuta macho wananchi.

Hata  hivyo wamesema sheria hiyo mpya itaweza kusimamiwa vyema  endapo wananchi wataendelea kutoa mashirikiano  hasa katika kuripoti kesi za udhalilishaji kwa wanawake na watoto au hata katika kutoa ushahidi mahakamani pindi wanapoitwa kuthibitisha  tukio.

Amina Omar Zanzibar24