Wafanyakazi wa Hospitali watakiwa kufanya kazi kwa kufuata sheria ilikupunguza ongezeko la watu wenye ulemavu

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamewataka wafanyakazi wa Hospital Nchini kufanya kazi kwa kufuata sheria na Taratibu za kazi zao ili kupunguza athari zinazopelekea Ongezeko la watu wenye ulemavu wa viungo.

Wakichangia hoja ya Mwakilishi wa Jimbo la Paje Jaku Hashim Ayoub kuhusu  kutopatikanwa kwa huduma Bora katika Hospital Kuu ya Mnazi Mmoja Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wamesema wananchi wamekuwa wakilalalmikia  matatizo mengi wakati utoaji wa huduma za Afya hospitali hapo ikiwemo kuengezeka kwa Uzembe wa madaktari.

Wamesema kuna baadhi ya madaktari wanasahau wajibu wao na katika kuwahudumia Wagonjwa na kuwasababishia matatizo ya Viungo wagonjwa waohitaji huduma za Afya .

Wamesema licha ya Serikali kuendelea kuimarisha upatikanaji wa Vifaa vya kutolea huduma kwa wagonjwa lakini baadhi ya madaktari wananchangia kurejesha nyuma Maendeleo ya Huduma za Afya inazokusudia kupatiwa wagonjwa Nchini.

Akijibu hoja za Wajumbe hao, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Raisi Muhammed Aboud Muhammed amesema Serikali itafatilia Suala hilo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Amesema kutokana na wananchi kuzidi kulalamika Mara kwa mara Serikali itaendelea kuwafatilia Madaktari wanaokiuka Maadili na Kazi zao ili kupunguza matatizo yanayojitokeza kwa wagonjwa.

Na:Fat-hiya shehe Zanzibar24.