Wizara ya fedha yafunguka juu ya Miradi ya wafadhili Zanzibar

Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar imesema hakuna matumizi mabaya ya Fedha za Miradi inayotolewa na wafadhili kwa njia ya ruzuku au mikopo kutoka Nnje ya Nchi .

 Akijibu swali katika kikao cha Baraza la wawakilishi Chukwani ,waziri wa fedha na Mipango Zanzibar Dk.Khalid salum  Muhammed  amesema Serikali na Taasisi husika zinafanya Uchambuzi na Ufatiliaji wa fedha zote Zinazotolewa ili kuziba mianya ya wizi wa fedha.

 Amesema tume ya mipango huandaa andiko la mradi na kuwasilisha Wizara ya fedha kupitia idara za nnje kwa ajili ya uhakiki na kupitishwa  ambapo miradi inayoanzishwa na wafadhili hushirikishwa jambo ambalo linapelekea kuondoa migogoro baada ya mikataba hiyo kuwekwa saini.

 Amesema serikali inaweka Miongozo na sheria ya kufuatwa katika miradi hiyo ili kuzuia Fedha za serikali zisipotee pamoja na kuzuia miradi hiyo kutokamilika baada ya kuazishwa.

Na: Fat-hiya Shehe Zanzibar24.