ZURA yatangaza bei mpya ya mafuta

Khuzaimat Bakari Kheir kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ,Nishati na Maji Zanzibar (ZURA) akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisi Maisara juu ya mabadiliko ya bei za mafuta ambazo zitaanza kutumika hapo kesho.(Picha na Kijakazi Abdalla   Maelezo Zanzibar.)
Mamlaka  ya udhibiti wa huduma za maji na nishati zanzibar ZURA imetangaza bei mpya ya mafuta kuanzia tarehe 13/2/2018.
Mkuu wa kitengo cha mahusiano ZURA huzaimat Bakari Kheri akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika Ofisi za mamlaka hiyo Maisara Mjini Zanzibar amefahamisha kuwa zoezi là alama kwenye mafuta kwa makampuni ya mafuta kujipanga vizuri kwa ukaguzi kwa lengo là kuzuia magendo ya uchakachuaji wa mafuta na kuhakikisha ubora Wa bidhaa za mafuta.
Mkuu huyo amefafanua kuwa bei ya mafuta  kwa mwezi huu wa  febuari 13 kwa mafuta petrol shilingi 2,256, diesel shilingi 2,175, mafuta ya taa shiling1,641 pamoja na mafuta ya bank  2,017
Sambamba na hayo amesisitiza kuifahamisha jamii kuwa hakùna uhaba wa mafuta na wasisikilize maneno ya watu mpaka watakapotoa taarifa mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati zanzibar ZURA.
Bei za mafuta zitaanza kutumika rasmin kesho tarehe 13/2/2018

Rauhiya Mussa Shaaban.