Kesi za madai yatalaka zaengezeka Zanzibar

Wizara ya nchi Ofisi ya Raisi Katiba sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora imesema kesi za madai ya Talaka zimeengezeka katika mahakama za kadhi ukilinganisha na kesi za madai ya matunzo ya watoto.

Akijibu swali katika kikao cha baraza la wawakilishi Chukwani,Naibu waziri wa Wizara hiyo Khamis Mwalimu amesema Mpaka sasa Jumla ya kesi za madai ya talaka kwa mwaka 2017 ni 884 ambapo mpaka sasa kesi kesi 440 zimetolewa maamuzi kwa Upande wa Unguja.

Kwa upande wa Pemba amesema jumla ya kesi 334 zimefunguliwa kati ya hizo kesi 249 zimepatiwa maamuzi kati ya kesi hizo 85 bado zinaendelea kusilizwa.

Akizungumzia kesi ya madai ya Matunzo ya watoto Naibu Khamis amesema takwimu zinaonesha kupungua kwa kesi ambapo kwa upande wa Unguja jumla ya kesi 35 kwa mwaka 2017 zimeripotiwa kati ya hizo kesi 17 zimeshatolewa maamuzi na 18 zinaendelea  kwa upande wa pemba kesi 22 zimeripotiwa kati yake 18 zimetolewa maamuzi na 4 zinaendelea.

Aidha Maalim ametowa wito kwa Wananchi kuendelea kutunza familia zao ili kuepusha Ongezeko la talaka kiholela pamoja na kuwakosesha watoto haki zao za msingi ikiwemo kupata Elimu.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.