Mwanasheria mkuu Kenya ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Prof. Githu Muigai amejiuzulu baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa miaka sita na nusu.

Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Prof. Muigai kwa kutumikia nafasi hiyo ambapo kwasasa nafasi hiyo itachukuliwa na jaji Paul Kihara. Kupitia ukurasa wake wa twitter Rais Kenyatta amethibitisha kujiuluzu kwa Prof Githu.

“Nimepokea kwa majuto uamuzi wa mwanasheria mkuu Githu Muigai. Namshukuru kwa huduma yake katika kipindi cha miaka sita na nusu. Nimemteua jaji Paul Kiharara Kariuki” ameandika Rais Kenyatta.