Watatu watiwa mbaroni kwakukutwa na Dawa za kulevya Unguja

Jeshi là polisi Mkoa wa Kusini Unguja jana 12 February 2018 limewashikilia vijana watatu, wawili waakazi wa paje Mkoa wa Kusini Unguja na mmoja  mkaazi wa Kwarara Wilaya ya Mgharib B Unguja wakiwa na kete za Dawa za kulevya kwa nyakati tofauti.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Kusini unguja Kamishna msaidizi Makarani Khamis Ahmed amesema kuwa mkaazi wa kwarara amekutwa akiwa na kete za dawa za kulevya 432 pamoja na vijana wawili waakazi paje wakiwa na kete 21 za dawa za kulevya.
Aidha Kamanda Makarani amesema kuwa bado wanaendelea kupambana na Dawa za kulevya katika mkoa huo,kwani lengo ni kupata mafanikio kwa kiasi kikubwa napia  kupunguza na kuondoa kabisa kadhia hiyo ya Dawa za kulevya.
Kamanda Makarani ametoa wito kwa jamii pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kusini kutoa ushirikiano na jeshi là polisi ili kutokomeza Dawa za kulevya.
Uchunguzi wa matukio hayo unaendelea kwani kesi hiyo tayari imeshakabidhisha mkemia mkuu kwa ajili ya uchunguzi ili kufikishwa mahakamani.

Na:Rauhiya Mussa Shaabani.