Zitto Kabwe amtembelea Mbwana Samatta nchini Ubelgiji

Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe jana Februari 12, 2018 alikwenda kumtembelea  Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta nyumbani kwake huko Genk nchini Ubelgiji.

Nilipata nafasi kumsalimu @samatta77 jana jioni nyumbani kwake Genk. Nimefurahi kuwa anaendelea vizuri na anapambana kuhakikisha anaendelea kukuza nchi yake na yeye mwenyewe. Ana mawazo mazuri Sana ya kuendeleza soka la Tanzania. Mungu atamsaidia Samata wetu Watanzania,” Ameandika Zitto kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kabla ya kumtembelea Samatta, Zitto alifanikiwa pia kumtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu anayeendelea na matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, nchini humo kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na risasi zaidi ya 36 na watu wasiojulikana, Septemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake eneo la Area D, Dodoma.