Kizee wa miaka 60 amlawiti mtoto wa miaka 8 Bwereu Unguja

Mzee mwenye umri wa miaka 60 amlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 8 huko Bwereu Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Baba mzazi wa mtoto huyo ameeleza kuwa “nikweli kuwa mwananangu jambo hili limemtokezea kwani tumesha mpeleka hospitali na madaktari wameshathibitisha kuwa amesha lawitiwa na anamichubuko ndani yake”

Kwahiyo mzazi huyo ameiomba Serikali pamoja na vyombo vya Sheria viweze kuchukua hatua kubwa ya kuvitokomeza vitendo hivyo.

Nae Sheha wa Shehia ya Bwereu Juma Nyange Omar amesema kuwa kutokana na matatizo yaudhalilishaji ameiomba jamii kushirikiana ikiwa mwananchi, sheha, askari pamoja ili kuweza kushikamana katika kupambana na tatizo hili.

“kinacho nisikitisha kuwa mzee wa miaka 60 kumfanyia tukio hili mtoto wa miaka 8  sio jambo jema kabisa kwahiyo sheria ichukue mkondo wake”amesema Sheha huyo.

Kwaupande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Hsina Ramadhan Tawfik amesema uchunguzi umeanza ameahidi kuwa wanashirikiana na jamii kuwa watamkamata mtuhumiwa na kuweza kifikishwa Mahakamni ili aweze kuendelea na kesi yake.

Kamanda Hasina ameishauri jamii kuwakaribu na watoto wao pamoja na kushauri jamii kuwa  itakapoweza kushuhudia matukio kama haya watoe ushahidi pamoja na mashirikiano ili mtuhumiwa aweze kukamatwa na kufikishwa Mahakamani.