SMZ yaombwa kuongeza ulinzi katika maeneo ya kitalii nchini

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweka ulinzi katika maeneo ya Vivutio vya watalii ili kuwawezesha watalii wanaotembelea vivutio hivyo kuendelea kuwa katika hali ya usalama na amani.

Wakiuliza maswali ya Nyongeza katika kikao cha Baraza la wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar ,Wajumbe hao wamesema Zanzibar ina sehemu nyingi zenye vivutio vya watalii lakini vivutio hivyo havina ulinzi wa kutosha.

Wamesema sehemu hizo zitakapo wekewa ulinzi na kuimarishwa kwa hali ya Usalama watalii wataongezeka na kuongeza upatikanaji wa mapato ya Nchi.

Kwa Upande wake Naibu waziri wa wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Chumu kombo Khamis amesema kutokana na umuhimu mkubwa wa watalii hapa Zanzibar Serikali italifanyia kazi Suala hilo ili kuimarisha vyanzo vya mapato ya Ndani.

Amesema Mwaka Uliopita Sekta ya Utalii ilifanikiwa kukusanya Shillingi million mia ambapo ni sawa na Shilingi Millioni 10 kwa kila mwezi kutokana na Vyanzo vya mapato ya ndani ikiwemo mapato yatokanayo na Matamasha mbalimbali ya Wanamuziki  na Watalii.

Naibu Chumu ametowa wito kwa wananchi kuthamini na kuvitunza vivutio vya kitaliii vilivyopo Nchini pamoja na kujenga utamaduni wa kuvitembelea ili kuongeza hamasa kwa wageni wanaotoka nje ya Nchi pamoja na kuchangia pato la Taifa.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.