Jinsi mwanamke anavyokurupuka katika mapenzi

Ikiwa leo ni siku adhimu ya wanawake duniani nimeweza kukuandalia makala fupi kuhusu njia tofauti ambazo wanawake wengi wanazozitumia katika kuyumbisha maisha yao.

Kwanza tunatakiwa tufahamu yakwamba Mwanamke ni yule ambae anaijua thamani yake tangu angali mdogo aidha kwa kufundishwa na wazazi wake au kwa utashi wake yeye mwenyewe binafsi.

Kutokana na maisha kila kukicha jinsi yanavyo endelea wanawake hujikita sana katika masuala ya kimapenzi pasi na kutathmini muelekeo bora wa kimapenzi.

Tutambue kuwa Mwanamke ameumbiwa mwanaume mmoja tu, mwanamke hatakiwi kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja, hutulia na mwanaume mmoja hata pale mahusiano yake yasipoenda sawia, husubiri muda muafaka wa kupata mwanaume atakaempenda na sio kuwapanga kwa msururu.

Baadhi ya wasichana hujijengea mazingira ambayo wao wenyewe wanahisi kuwa ni muafaka kwa maisha yao hususan katika mahusiano.Hebu tuweze kuwafahamu wanawake ambao hukosea katika suala zima la mahusiano.

1  Kuwa na matarajio makubwa sana aingiapo katika mahusiano, kuwa na matarajio makubwa                    kuhusu ndoa. Na mara aingiapo katika ndoa hukuta mambo sivyo kama alivyotegemea.

 

  1. Kuvaa nguo fupi zinazoonesha maungo yao, mwanaume anaejielewa hawezi kuoa mwanamke wa namna hiyo. Kwake ataona utafaa zaidi kama ukiwa mchepuko.

 

  1. Kupenda pesa kupitiliza! ni kweli mwanaume anawajibika kumhudumia mwanamke, lakini ikifika kipindi wewe unawaza hela tu, mwanaume akikuambia hana hela umenuna. Kamwe hawezi kufikiri kukuoa. Utachezewa ili kuhakikisha pesa zake zimeenda halali na kuachwa.

 

  1. Kuwa na masharti magumu kuhusu mwanaume unayetaka akuoe. Baadhi ya wanawake wana masharti magumu utafikiri fomu za mikopo ya benki ambayo inakaribia kufilisika. Mimi nakuhakikishia utagonga miaka 35 bado bila bila.Unakuwa na vigezo vingi utafikiri wewe ni mkamilifu asilimia 100.

 

  1. Kulengesha mimba huku ukidhani itakuwa njia nyeupe ya wewe kuolewa. Hili ni kosa kubwa sana ambalo limeibuka hivi karibuni.

Wengi hudhani kuwa ukibeba mimba yake lazima atakuoa. Sawa anaweza kukuoa ila machungu             yake utakayoyapata baada ya kuingia ktk Ndoa utaomba half time mwenyewe.

 

  1. Kupenda kujionyesha na kujikweza uonekane jinsi ulivyo wa gharama, sawa inawezekana ni wa gharama kweli ila hata wanaume wa gharama wapo vile vile.Utaishia kuchezewa na kuachwa pamoja na kucheza kwaito kwenye Ndoa za wenzako. Na itakubidi ukumbuke muda haukusubiri wewe. Mwanamke ajikwezae hana busara kabisa.
  1. Kutembea na waume za watu na vibabu vilivyostafu vinavyokula pensheni. Hiyo ni laana. Unajifungia baraka za kupata mume bora. Au utaweza kupata mume ila malipo ya uliyokuwa ukiyafanya lazima uyapate hapa hapa Duniani.

 

  1. Utoaji wa mimba! Hili najua linafanywa na wengi sana na limekua janga kubwa sana. Laana ya umwagaji damu au kuua ni kubwa mno. Starehe ulipata na ukafurahi kabisa kuwa amekufikisha sasa iweje mimba uje uitoe? Kama umefanya hivyo nenda katubu kwa muumba wako na kama hujawahi basi kamwe usithubutu. Kila mtoto huja na baraka zake.

 

  1. Pesa pesa pesa!! Narudia pesa isiwe kigezo chako cha kumpenda mtu, unamkataa leo kwa vile hana pesa ila kumbuka ana utajiri wa mapendo na hawezi kuwa masikini milele.Utajiri ni jitihada tu. Ungana nae mpe moyo, pesa ni rahisi kuzipata kama ukizitafuta ila upendo wa kweli ni ngumu kuupata.

 

  1. Kumbuka Maisha hayajawahi kuwa salama kwa msaliti, leo hii umewapanga foleni lakini   ukumbuke kuwa hautaishi maisha kama hayo miaka yote.Ipo siku na wewe utabanwa katika   kona na utatamani utoweke duniani, lakini hutatoweka ila cha moto utakiona.

11.  Miaka ikikatika na akifikiasha umri wa miaka 30+ na bado bila bila, husema anahitaji mtoto tu               na hana haja ya mume, lakini akiwa mwenyewe chumbani kwake, anajijua na nafsi yake jinsi                   anavyotamani maisha mema ya ndoa.

12. Wanawake wengine Utetezi wao mkubwa wao husema ndoa kitu gani, watu wanaoana leo na                   wanaachana kesho, pasina kujua kwamba Ndoa inahitaji msingi imara ikiwemo na uvumilivu.

Ni vigumu sana kushindana na asili, kuna wakati utafika na kusema bora ningefanya hivi. Amua njia ile iliyo sahihi ambayo kwako unajiona hutakua na majuto nayo hapo baadae.

Siku zote kuna manufaa katika kusubiri, ila kuna majuto mengi katika kukurupuka.

Mungu awabariki ‘wanawake’ wote katika magumu yote wanayopitia na aweke wepesi kwakila mazuri na pia awabariki ‘wasichana’ watambue ni nini wanapaswa kufanya, kwa muda muafaka na maisha yao.

Itambue Kauli Mbiu ya mwaka huu 2018 kwamba:Kuelekea Uchumi wa Viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.

 Siku ya wanawake ilianza mwanzoni mwa mwaka 1900 kwakupitia wafanyakazi wanawake wa Sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii kwa kuwepo na vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku hiyo ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbali mbali yanayohusu haki na ustawi wa wanawake.

Tatu Juma na Zanzibar24.