Njia 6 za kuondoa ukavu wa miguu na kuifanya kuwa laini

Watu wengi hutamani kuwa na nyayo za miguu laini nzuri zenye kuvutia kwenye macho ya watu lakini inashindikana na kujikuta wakiwa na nyayo kavu zisizovutia kuonekana machoni mwa watu.

Kwa kawaida ngozi ya kwenye nyayo huwa ni kavu ukilinganisha na ngozi ya maeneo mengine mwilini lakini mwanamke au mwanamume mwenye kujali muonekano wake hadharau afya ya ngozi ya miguu yake.

Vitu vinavyosababisha ukavu mpaka kupasuka nyayo ni:

1.Kutembea sana peku.
2.ukali wa jua na miguu unaikanyaga chini.
3.Kuogea sabuni ambazo hazina moinsture.
4.tatizo la kisukari na thyroid.
5.kuogea maji ya moto kupitiliza kila siku.
6.matatizo ya ngozi eczema ambayo hupelekea ngozi kuwa kavuu.

Unatibu vipi ukavu wa nyayo?  fuata njia moja miongoni mwa zilizoorodheshwa hapo chini  au zote kadri uwezavyo?

1.Osha miguu yako kwa maji safi na sabuni kisha ikaushe, hakikisha unapaka nyayo zako mafuta au lotion zenye moinsture.Usipake lotion zenye kemikali au alcohol huzidisha ukavu wa miguu.Paka hata mafuta ya watoto ambayo hayana kabisa kemikali.

2.Unaweza kuroweka miguu yako kwenye maji ya uvugu uvugu uliyoyakamulia maji ya limao kwa dakika tano kusaidia kuondoa zile dead skin kisha ikoshe vizuri na upakae mafuta ya vasseline.


3.Paka miguu yako mchanganyiko wa kijiko kimoja cha olive oil na matone kadhaa ya limao.Changanya vyema kisha paka kwenye nyayo ili kuipa moinstrure yaani unyevu unyevu.
4.Unaweza kutengeneza scrub yenye mchanganyiko wa unga wa mchele,olive oil,veniger na asali.Unazifanyia scrub nyayo zako na huo mchanganyiko.
5.Ukishasafisha na kufuta miguu yako paka vegetable oil…mafuta kama hayo ya olive na mafuta natural kabisa ya nazi.

Mafuta ya Nazi

6.Kabla ya kulala Chukua mafuta ya vaseline ujazo wa kijiko kidogo cha chai na kamulia limao zima kisha koroga vyema huo mchanganyiko kisha paka kwenye nyayo zako.Fanya hivi ukiwa umenawa miguu na umeifuta vizuri imekauka ndio unapaka.Vaa socks zako ndio upande kitandani kulala.

 Kumbuka ni muhimu kumuona daktari hasa kama una hali mbaya kwa ushauri na matibabu zaidi.Na pia kama hali hiyo inatokana na magonjwa niliyoyataja hapo juu.