Awaua watoto 3 wa mke mwenziwe kisha nae kujinyonga

Mwanamke mmoja katika kijiji cha Nyahera Kaunti ya Kisumu nchini Kenya, amewaua watoto watatu wa mke mwenzie, na kisha mwenyewe kujinyonga.

Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki hii ya tarehe 11, Machi, ambapo limeelezwa kwamba mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Jacinta Otieno, aliwaita watoto hao ambao walikuwa wanne kwenda kunywa uji nyumbani kwake, na ndipo alipoanza kuwacharanga na mapanga mpaka kuwaua na kisha mwenyewe kujinyonga, huku mtoto mmoja akinusurika baada ya kukataa kwenda kunywa uji.

Jacinta alifanya tukio hilo baada ya mke mwenzie kwenda kanisani na kuwaacha watoto peke yao nyumbani ambako wanaishi jirani, huku mume wao akiishi jijini Nairobi na watoto wawili ambao amewazaa yeye.

Kwa mujibu wa majirani wawili  wameeleza kuwa hawakuwa na maelewano mazuri kutokana na wivu kwa mume wao, na kwamba Jacinta alishajaribu kutaka kujiua wiki moja iliyopita.

Watoto hao waliouawa walikuwa na umri wa miaka 7, 4 na 2, walikuwa wa mke mwenzie Hellen Otieno.