Kituo cha Afya Michenzani Pemba chaleta faraja kubwa kwa wananchi

Imeelezwa kwamba kuwepo kwa kituo cha cha Afya daraja la pili katika Shehia ya Michezani Wilaya ya Mkoani pamoja na upatikanaji wa dawa kwa uhakika  kumeweza kuwaondosheha usumbufu mkubwa wananchi wa shehia hiyo na vijiji jirani zikiwemo huduma za mama waja wazito na watoto

Wakizungumzia uwepo wa kituo hicho na huduma zinazopatikana wakaazi wa vijiji cha Chokocho , Michenzani na  Stahabu wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ujenzi wa kituo hicho.

Wamesema kwa sasa wanapata huduma hizo ndani ya masafa mafupi ambapo kabla ya hapo huduma hizo walikuwa wakizifuata katika hospitali za mbali zikiwemo za Bogoa, Stahabu na Abdalla mzee Mkoani.

Licha ya wananchi wa vijiji hivyo kupongeza huduma zinazotolewa na kituo cha afya Michezani Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mohamed Faki Saleh amesema pamoja na upatikanaji wa dawa katika kituo hicho lakini tatizo kubwa linalokikabili kituo hicho ni uchache wa wafanyakazi.

Amesema kituo kituo kimekuwa kikitoa huduma za aina mbali kikiwa na wafanyakazi watano na ili kituo hicho kiweze kufanyakazi zake kwa ufanisi zaidi kinahitaji kuwa na wafanyakazi wasiozidi kumi na saba.