Madereva wa Ambulance wapewa onyo kali na Jeshi la Polisi Zanzibar

Jeshi la Polisi limetoa tahadhari kwa madereva wa gari za kuchukulia wagonjwa (Ambulance) kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria za barabarani kwa usalama wao binafsi na jamii iliyowazunguka

Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharib Unguja Hassan Nassir ametoa tahadhari hiyo huko ofisini kwake Madema wakati akizungumza na waaandishi wa habari.

Amesema kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani hakuna gari ya Ambulance inayoruhusiwa kuvunja sheria yoyote ya barabarani huku akisema watawachukulia hatua madereva wa gari hizo pindi wakikiuka sheria hiZo.

Kamanda Nassir ametoa tahadhari hiyo kufuatia malalamiko aliyoyapokea juu ya uvunjifu wa sheria za barabarani Unaofanywa na madereva wa Ambulance ikiwemo kupita njia iliyokuwa si yao, kutopunguza mwendo iwapo mtu anakatisha barabara kwa kutokukisikia king’ora hali inayohatarisha uhai wa watu wengine.

Kamanda nassir amesema lengo la kuwekewa kingora gari hizo ni kuwajulisha watumiaji wengine wa barabara kuwa kuna mtu amepata maafa hivyo wanaombwa wakae pembeni ili kuruhusu mtu huyo kuwahishwa kupatiwa matibabu na si kuwasababishia maafa watu wengine.

Kamanda Nassir ametoa wito kwa madereva hao kuwa na tahadhari wakiwa barabarani kwani jeshi la polisi halito wavumilia sheria kali zitachukuliwa dhidi yao endapo wakihusika na uvunjifu wa sheria za barabarani.