Skuli ya fukuchani ya zorota ufaulu wa wanafunzi sababu ni hii

Kuwepo kwa ajira  kwa watoto chini ya maika 18 na kuendelea  kumechangia  kwa baadhi ya wanafunzi wa skuli ya fukuchani kukatisha masomo yao  na kujiinza katika ajira za utotoni ikiwemo  uvuvi na ubanjaji kokoto.

Akizungumza na Zanzibar24  Kaimu Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Fukuchani  Hamza Ali Hamdu  amesema wanafunzi wengi hasa wakiume wamekuwa hawahudhurii skuli  badala yake wanatumia wakati wa skuli kwenda kwenye vibarua na kujikosesha haki zao za  msingi ya kupata elimu.

Amesema  kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo la utoro hivi sasa kamati ya skuli kwa kushirikiana na Polisi jamii pamoja na Sheha wanampango wa  kufanya msako kila nyumba katika kijiji cha fukuchani  kuwatafuta wanafunzi walio acha masomo yao kisa ajira za utotoni kuwarudisha skuli ili kuendelea na masomo.

Aidha Hamza amesema  uwepo wa  bahari karibu na  kijiji hicho  unachangia vijana wengi  kujishughulisha na kazi  za uvuvi hivyo elimu inahitajika kwa  wazazi katika kuwadhibiti watoto wasijiingize katika ajira za utotoni.

Amesema skuli yake imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani yake hasa ya darasa la kumi lakini utoro  kwa wanafunzi  umekuwa ukizorotesha  hali ya ufaulu hasa kwa wanafunzi wa darasa la kumi  na mbili.

Hivyo ametoa wito kwa wazazi kushirikiana na walimu wa skuli hiyo katika kuwarudisha watoto skuli kwani ajira za utotoni hazina tija badala yake  ni kupoteza wakati kwani bila ya elimu kichwani sawa sawa na sifuri.

Skuli ya fukuchani ni miongoni mwa skuli zilizopo katika Mkoa wa kaskazini Unguja Wilaya ya kaskazini A.

Amina Omar