Ukosefu wa viwango bora vya matairi yapelekea ajali nyingi barabarani

Watumiaji wa vyombo vya moto wametakiwa kuwa makini  wanaponunua matairi ya magari  kuhakikisha   yanakuwa na viwango  ili kulinda usalama wa raia na  ajali za barabarani.

Akizungumza na Zanzibar24  Afisa kutoka Taasisi ya Viwango Zanzibar ZBS  Muhtari Chande amesema  ongezeko la ajali barabarani linachangiwa na ukosefu wa viwango kwa matairi yanayotumika  katika vyombo vya moto hivyo ili kunusuru ajali hizo nivyema  watumiaji kufata sheria zilizowekwa.

Amesema taasisi ya viwango Zanzibar haita mvumilia mtu atakae bainika ananunua au kutumia vitu vilivyokuwa havina viwango na lengo kuu ni kulinda usalama na afya za  wananchi.

Aidha amesema hivi sasa Zanzibar imekuwa na uingizwaji mkubwa wa matairi na mengi yao hayana viwango jambo ambalo linachangia  kuonekana Zanzibar ni jaa  la takataka.

Hata hivyo amewataka watumiaji wa vyombo vya moto  kuhakikisha wanaponunua matairi yanaendana na viwango vilivyowekwa na ZBS na kuwa makini katika kufuata sheria zilizowekwa kwani  hatua hiyo itasaidia kuepusha ajali pamoja  na utunzaji wa mazingira.

Amina Omar