Wananchi wa magharib ‘A’ wametakiwa kuhama kwa usalama wao

Mkurugenzi wa baraza la Manispaa la Magharib ‘A’ Said Juma Ahmada amewataka  wananchi  kuacha kujenga katika laini kuu za kupitia umeme ili kuepusha athari zitokanazo na umeme.

Akizungumza na Zanzibar24  amesema wamebaini  kuna baadhi ya wananchi wanajenga katika laini kuu za umeme  jambao ambalo ni hatari kwa usalama wao na si haki kisheria maeneo hayo  kufanyiwa ujenzi  hasa nyumba za makaazi na kutoa  wito wananchi waliobainika kuondoka mara moja katika  maeneo hayo.

Hata hivyo Said ametoa wito kwa wale waliolipwa na serikali  kwa ajili ya kusitisha kufanya shughuli za ujenzi kuacha kujenga katika maeneo hayo  na kuondoka  kabla hatua za kisheria  hazijachukuliwa.

Aidha amesema ni vyema  wananchi wakahakikisha wanafata mipango miji pindi wanapotaka kujenga ili kuepusha migogoro ya kubomolewa nyumba zao hali ambayo inawapa hasara kubwa hasa ukiangalia  na hali ya ugumu wa maisha.

Amina Omar