Wema Sepetu: Dawa zinaniponza

Malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameweka wazi kuwa dawa anazotumia ndizo zinazomponza hadi kuwa na mwili mkubwa ambao yeye mwenyewe haupendi na kudai kuwa anatamani kuziacha ili mwili wake uweze kupungua.

Wema Sepetu ameweka wazi hilo kupitia mtandao wa kijamii wa Instgram wakati akimjibu msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Ray C ambaye amefanikiwa kupunguza mwili wake na kurudi kwenye ubora wake kama zamani.
Ray C alikuwa akiwakumbusha Shilole pamoja na Wema Sepetu kuwa wanaweza kupunguza miili yao na kilo na kuwa kama zamani kwa kujitolea mfano yeye.

Kufuatia kauli hiyo ya Ray C ndipo mwanadada Wema Sepetu alipoamua kuweka wazi kuwa si mapenzi yake yeye kuwa na mwili huo alionao sasa bali ni kutokana na matumizi ya dawa, ambazo hakuweka wazi ni dawa zipi, ingawa baadhi ya mashabiki wameunganisha na kudai kuwa huenda msanii huyo anatumia dawa zitakazomsaidia ili aweze kuja kushika ujauzito, huku wengine wakisema ni matumizi ya dawa za kupunguza mwili.

“Yaani mimi sielewi jamani siyo mimi dada yangu…Dawa zinaniponza mimi na naziacha” aliandika Wema Sepetu

Baada ya jibu hilo Ray C alirudi tena na kumpa pole Wema Sepetu na kumweleza kuwa hakuna namna tena inabidi azikate ili aweze kupungua na kudai kuwa inawezekana kabisaa Wema Sepetu akarudi kama zamani endapo atazingatia mafunzo, mpangilio mzuri wa chakula na kusema kabla ya mwaka atampa matokeo ya hilo.

“Pole wangu inabidi uzikatie tu hakuna namna, inawezekana kabisa yaani niamini mimi !a good trainer! proper diet! less than a year utaniambia! uamuzi tu, najua unaweza Wema Sepetu”alisema Ray C.