Baraza la manispaa latoa tahadhari kwa wafanyabiashara wa vyakula Zanzibar

Wafanyabiashara wa vyakula Zanzibar wametakiwa kuwa makini katika kipindi hichi cha mvua zinazoendelea kunyesha kuhakikisha katika maeneo yao wanayouzia biashara  yanakuwa safi na salama ili kulinda afya za wananchi.

Akizungumza na Zanzibar24  Mkurugenzi wa baraza la manispaa la Magharib ‘A’  Said Juma Ahmada amesema endapo wafanyabishara  hawatokuwa makini katika  suala la usafi  wataweza  kusababisha  ugonjwa wa kipindupindu  zanzibar kwani kuna baadhi ya wafanyabiashara  hawafuati sheria zilizowekwa na baraza la manispaa na Wizara ya afya Zanzibar.

Amesema  lazima  wananchi wafuate sheria zilizopo hususani wauza vyakula na endapo  watakaidi  baraza la manispaa halitamvumilia mtu  na kwa hatua za awali watamfungia biashara yake  ili kuepusha  maradhi ya miripuko ikiwemo kipindupindu.

Aidha Said amesema elimu zimekuwa zikitolewa mara kwa mara juu ya maradhi hasa katika kipindi hichi cha mvua na kuwataka wananch nao kuzidisha usafi katika makaazi yao  ili kulinda mazingira.

Amina Omar