Irene Uwoya ajibu mapigo baada ya mumewe Dogo Janja kutangaza kuongeza mke

Mke wa msanii wa muziki Dogo Janja, Irene Uwoya ametoa majibu juu ya habari zilizozagaa kuhusu mumewe kutaka kuongeza mke wa pili hadi wanne.

“Ndoutajua mim Kabila gani…thubutu uwone tena wasikudanganye @dogojanjatz,” ameandika Irene Uwoya katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram mapema leo baada ya kuona stori za mumewe za kumuongezea mke zikitawala.

Katika kipindi cha The Playlist ya Times Fm kilichoruka juzi ( 12-03-2018) mkali huyo wa ‘Wayu Wayu’ alidai kuwa anampango wa kuongeza mke wa pili hadi wanne kila baada ya miaka 10.