Madaktari wasipo kuwa wapole na maneno ya busara kwa wagonjwa kibarua chao kitaota nyasi

Watendaji  wa wizara ya Afya  zanzibar  pamoja wauguzi  katika Hospitali ya Mnazi Mmoja  na vituo mbalimbali vya afya wametakiwa  kufanya kazi kwa uwadilifu na unyenyekevu  pamoja na  kuwa na maneno ya busara kwa  wananchi wanaofata huduma  na endapo  wakiwabaini  wanafanya kinyume na hilo wataachishwa kazi.

Akizungumza na Zanzibar24  Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed amesema kumekuwa na malalamiko  mengi kwa wananchi kutorizika na  utendaji  wa wizara hiyo , hivyo ili kuondoa malalamiko hayo lazima  watendaji wawajibike  kikamilifu bila ya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Amesema Serikali inatambua kuwepo kwa upungufu wa  madaktari lakini watendaji wasichukue kigezo hicho cha kuwacha kuwajibika katika majukumu yao na wakumbuke kuwa kazi ya kuwahudumia wananchi ni ya mashirikiano.

Hata hivyo  Hamad amesema mbali na hayo pia lipo tatizo kwa baadhi ya watendaji kuuza  bidhaa za serikali ikiwemo dawa jambo ambalo nikinyume kisheria  kwani  dawa hizo serikali inazitoa bure kwa wananchi hivyo  nivizuri kwa kila mwenye  zamana kusimamia zamana yake na kuwacha tabia hizo mbaya zinazoichafua Wizara ya Afya.

Amina Omar