Rayvanny afunguka kuhusu kufunga ndoa

Baada ya Diamond kuomba baraka kwa mama yake kuhusu kufunga ndoa mwaka huu, naye Rayvanny amedokeza kuhusu suala hilo hilo la ndoa.

Dokezo hilo la ndoa limekuja  wiki chache baada ya msanii huyo na mpenzi wake kurejea kutoka  Mkoani Mbeya, nyumbani kwa akina Rayvanny.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Ray aliweka picha yake akiwa katika vazi la suti na kuandika “Bwana Harusi” naye mpenzi wake Fayvanny hakubaki nyuma na akuamua kujibu kuashiria wapo katika michakatao hiyo ya ndoa.