Uwepo wa mswada wa kisheria utakuwa mkombozi kwa wananchi wanyonge

Wadau wa masuala ya kisheria wametakiwa kutumia vyema taalum zao katika kutoa  huduma bora  za msaada wa kisheria kwa wananchi  ili  kwenda sambamba na lengo la serikali ya mapinduzi Zanzibar katika kuleta mabadiliko  kwa jamii hususani wanyoge.

Kauli hiyo ameitoa Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria Jaji Mshibe Bakari wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili sheria ya msaada wa kisheria amesema lazima wadau wa sheria wajikubalishe kufanya kazi kwa bidii na weledi  ili kuondoa malalamiko kwa wananchi kwani imebaini  wananchi wamekuwa wakiingia katika makosa kutoka na kushindwa kujua sheria  na kushindwa kujitetea wanapofikishwa mahakamani hivyo wadau wa sheria  wametakiwa kuwacha tama za fedha badala yake kufanya kazi kwa usawa.

Mshibe amesema wapo baadhi ya wananchi  hususani wanyoge wamekuwa wanatiwa hatiani  na kuhukumiwa  kifungo  kutokana na  kushindwa kutoa ushahidi  mahakamani hivyo uwemo wa mswaada huo wa kisheria utawasaidia katika kuwatetea wananchi ambao hawaweze kujitetea mbele ya mahakama.

Amina Omar