(ZFA) yatoa adhabu kwa timu 3 Zanzibar

Chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) kimetoa adhabu kwa kwa timu tatu zinazoshiriki ligi kuu Zanzibar kanda ya unguja kwa kosa la kuingia uwanjani   kwa kupitia mlango usiostahiki kuingilia kwa wachezaji uwanjani.
Adhabu hizo zilitolewa kwa timu ya Black sailors, Miembeni city na kilimani city ambapo kila timu inalazimika kulipa faini ya shilingi laki moja mara baada ya kubainika kutenda kosa hilo.
 Akizungumza na waandishi wa habari za michezo visiwani Zanzibar Afisa habari wa chama cha soka visiwani Zanzibar ZFA Ali Bakari cheupe alisema ZFA imezitoza faini ya shilingi laki moja kwa kila  timu  kutokana na kubainika kufanya kosa la kuingia uwanjani kinyume na mlango uliopangiwa kuingilia wachezaji ambapo vitendo hivyo vimekithiri kufanywa na timu nyingi visiwani Zanzibar.
“ kwa mujibu wa kanuni za kuendeshea mashindano ni marufuku kwa timu kupita katika milango ambayo haiusiki  kuingilia uwanjani hivyo ZFA imefiakia maamuzi hayo   ili kukomesha vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya timu ambavyo vinaonekana vimekithiri” alisema cheupe afisa habari wa ZFA.
Vitendo vya timu mbali mbali kukaidi kuingilia uwanjani kupitia mlango usiostahiki huwa unahusishwa na Imani za kishhirikina katika soka.
Pia alisema kwa upande mwingine chama cha mpira wa miguu viwani Zanzibar ZFA kimemchukulia hatua za nidhamu kocha msaidizi wa timu ya kilimani city Abrahamani Mussa kutokana na kosa la kuwatolea maneno ya kashfa waamuzi waliochezesha mchezo kati ya timu ya kiliamni city dhidi ya black sailors.
 Aidha alisema ZFA imefikia maamuzi ya kumtaka kocha huyo msaidizi wa kilimani city kuto kaa kwenye benchi la ufundi kwa muda usiojulikana mara baadaya kubainika kuwa ametenda vitenda vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kuwatolea maneno ya kashfa waamuzi.
Hata hivyo alisema pindi kocha huyo atakapo kaidi kutumikia adhabu hiyo aliopatiwa chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) basi timu nzima kiliamani city itawajibika.
“kitendo kilichofanywa na Abrahamani mussa kocha wa kilimani city ni kinyume na maadili ya kocha hivyo kwa maamuzi yaliochukuliwa na ZFA ni kama onyo Kali ili mwingine asije fanya kosa kama hilo” alisema cheupe.
Vitendo vya utovu wa adabu vimekuwa vikiripotiwa kwa wingi katika soka la Zanzibar ambapo hulitia dosari soka visiwani humo.
Na. Thabit Madai.