Wanafunzi wa Skuli ya sekondari ya Mtule watoa wapeleka ombi kwa Wizara ya kilimo

Wanafunzi wa Skuli ya sekondari ya Mtule wameitaka Wizara ya kilimo, Mali Asili ,Mifugo na Uvuvi kuandaa utaratibu maalumu utakao wawezesha wanafunzi waliozungukwa na Msitu wa jozani kwenda kujifunza katika msitu huo bila ya kutozwa fedha ili waweze kujifunza namna ya kuhifadhi Mazingira.

Wakizungumza na Zanzibar24 baada ya kupanda miti katika eneo la skuli yao Wamesema uhifadhi wa misitu unahitaji mashirikiano makubwa hususan kwa wananchi waliozunguka msitu huo hivyo watakapo andaliwa mazingira ya kujifunza katika msitu huo itawawezesha kutowa elimu juu ya athari ya uharibu wa misitu unaofanywa na baadhi ya watu.

Aidha katika kuelekea siku ya kilele cha Misitu Nchi wanafunzi hao wametowa wito kwa wanafunzi wanaomaliza masomo yao kuacha kujihusisha na tabia ya ukataji miti ya misitu kinyume na sheria badala yake wajiendeleze kitaaluma ili waweze kujiajiri wenyewe hususan katika Ufugaji na kilimo.

Naibu katibu ya Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira ya Jozani na ghuba ya Chwaka JECA Awesu Shaaban Ramadhani amesema licha ya kuwepo kwa wanannchi wanaoharibu mazingira kwa maksudi JECA itahakikisha inarejesha miti ya asili ili kuiweka Zanzibar katika haiba Nzuri.

Amesema wamekusudia kupanda miti katika maeneo mbali mbali ya skuli na katika Maeneo ya hifadhi ya Msitu yaliyoathirika na majanga ya moto ili kurejeresha rasilimali za misitu Nchini na kutowa wito kwa wananchi kutumia vyema kipindi cha mvua za masika katika kupanda miti.

Nae Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya  Jozani na Huba ya Chwaka  Ali Mwinyi amesema wataendelea kushirikiana na wananchi katika kulinda rasilimali ya misitu ili kuimarisha utalii kwa wageni waotembelea Zanzibar.

Aidha amesema katika kwaondoshea usumbufu wanaoupata wananfunzi waliozunguka msitu huo wakati wakihitaji kutembelea msitu huo amesema watahakikisha wanaandaa mazingira ya kuwaruhusu wanafunzi hao kunufaika na elimu ili kujua historia ya misitu huo pamoja na athari za ukataji miti ovyoo.

Aidha ametowa wito kwa vijana kutumia mbinu m,badala ya kuweza kujiajiri ili kuachana na tabia ya kukata miti kinyume na sheria .

Siku ya misitu inatarajiwa kuadhimishwa kesho ambapo kwa Zanzibar siku hiyo itaadhimishwa katika Ukumbi wa baraza la wawakilishi la Zamani Mjini Unguja ikiwa na ujumbe usemao MISITU ENDELEVU KWA MAENDELEO YA MIJI.

Zanzibar24.