Utafiti: Sababu 3 za mabadiliko ya majina ya Wazanzibari kutoka kale hadi sasa

Wahadimu ni watu waliokuwepo na kueka maakazi awali Zanzibar kabla ya miji mingine ya Kiarabu kwenye Pwani ya Mashariki ya Afrika.

Iyo miji ilikuwa ni kidogo zaidi kuliko ile ya Pate na Kilwa. Kama wakati wa utawala wa Sultani Omar kisiwani Zanzibar kwa hapo awali (karne ya 13), “Zanzibar haikuwa na umaarufu”.

Hii ni dhahiri kwamba wakati Waarabu na Waajemi walipofika Zanzibar, inaonekana waliwakuta watu tayari wakiwa wanaishi, na hao watu walijulikana kama “Wahadimu

Jina lao labda lilitokana na Waarabu (خدم) “mtumishi“. Walioishi vijiji vya ndani vya Kisiwa cha Zanzibar wakiwa kama wavuvi na mkulima ambao walikuwa wakitumia lugha zao wenyewe.

Kuna dalili nyingi, badala ya mila yao ya kikabila kwamba walikuja kutoka Saadani na Bagamoyo. Lakini wakuu wao katika miaka ya 1870, wanaonekana kuwa wa asili ya Kiajemi, kama wale wa Kilwa, Vumba nk.

Asili ya Makabila ya Wazanzibar, ni tatu; Wahadimu, Watumbatu na Wapemba.

Wahadimu hawakuwa wakisafiri mara kwa mara kutokana na shughuli zao za kilimo Isipokuwa kwa wachache ambao walikuwa wavuvi ingawa walisafiri kwenda Pemba wakati wa kuchukua karafuu.

Baadhi ya tamaduni za Wahadimu ni: Kilimo, uvuvi, uwindaji, kuabudu, Ndoa na kuzaliana.

Historia hii inapatikana kwenye kitabu cha Journal of African Society, July 1916, Vol. 15, No.60,  pp.356.

 

MAJINA YA WAHADIMU: KABLA YA KUINGILIANA NA WAGENI 

Majina yao yaligusia Mazingira yaliyowazunguka / asili yao Mpini, Shoka, Kishuke, Kinama, Kipevu, Kona, Kibibi, Panya, Buku, Matogo, Kijibwe, Kijiti, Choko, Mbaazi, Chausiku, Kipunda, Mwaka, Hamba, Ndumbu, Semeni, Sikudhani … 

 WAKATI WA KUINGILIANA NA WAGENI KWA MARA YA KWANZA (WAARABU, WAAJEMI, WAISLAMU) 

Majina yao yalianza kubadilika hususani kwa watoto wao. Majina ya mseto / mchanganyiko; mabadiliko na kuiita Haji Mcha, Daudi Shika, Msa Kinole, Issa Buzi, Ame Mjundu, Ali Maneno, Mariam Hodi, Abdalla Kichome, Kheri Mbingu, Abdalla Cheusi, Issa Pira, Makame Pungua … 

USHAWISHI WA MOJA KWA MOJA WA “WAGENI KUTAJA MAJINA” KWA WAHADIMU. WALIANZA KUPOTEZA MOJA YA ISHARA MUHIMU YA UTAMBULISHO WAO.

 Je, ni ushawishi wa Kiislamu, ushawishi wa Kiarabu au ushawishi wa Kiajemi? Baadhi ya majina: Khadija, Zainab, Mustafa, Jihad, Madina, Baraka / Mbaraka, Neema, Subira, Miraji, Ramadhani, Hija, Uwesu, Ali, Muhammad, Abubakar…

USHAWISHI WA MOJA KWA MOJA WA UTANDAWAZI, TEKNOLOJIA, (ICT)! 

Wanatafuta majina kutoka kwenye tovuti na Dictionaries. Wao wanawaita wasomi wa Kiislam na kuwaomba kuchagua majina mema kwao au watume kwa wachungaji faili ya majina na walichagua kwa niaba yao:  Mulhat, Umaymat, Ulfat, Shaharzad, Niiliyn, Musayyar, Mukatabat …

Dkt. Issa H. Ziddy