Mh. Samia: Kila mwananchi anahitaji kushirikishwa katika shughuli za kuleta maendeleo

Wazazi na walezi wametakiwa kutowaficha watoto wao wenye Ulemavu wa Viungo ili waweze kunufaika na haki zao za Msingi ikiwemo kupata Elimu na kushirikishwa katika  shughuli za miradi ya Maendeleo.

Akizungumza Baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Osifi ya Watu wenye Ulemavu Shaurimoyo Mjumbe wa Kamati ya Chama cha Mapinduzi CCM Samia Suluhu Hassan amesema watoto wenye ulemavu wanahitaji kunufaika na huduma hizo hivyo si vyema kuendelea kuwekwa ndani.

Amesema kila mwananchi anahitaji kushirikishwa katika shughuli za kuleta maendeleo ya Nchi katika kuimarisha Uchumi ulipo hivyo watakapo shirikishwa wataweza kunufaika na elimu kwa lengo la kuwaandalia Mazingira ya kuweza  kujiajiri na kuondokana na utegemezi katika familia zao.

Amesema watu wenye ulemavu wanauwezo mkubwa wa kuchangia mapato ya nchi pindipo wataandaliwa mazingira rafiki kuanzia katika familia zao na Serikali kwa ujumla.

Wakati huo huo Mjumbe huo ambae pia ni Makamo wa Raisi wa Serikali ya Jamuhuri ya  Muungano Tanzania,amekagua Mradi wa Ujenzi wa Tawi la CCM Jang’ombe Urusi na kuwataka wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM kuendeleza Mashirikiano na kukithamini Chama hicho ili kiendelee kudumu madarakani.

Amesema uhai wa chama unatoka na mashirikiano mazuri kati ya Viongozi na Wananchi hivyo ni vyema kuendelea kutoa elimu juu ya Umuhimu wa Chama cha Mapinduzi kwa watoto wao pamoja na kulinda mali za Chama ili ziweze kuwaletea maendeleo wananchi.

 Mh.Samia amemaliza Ziara yake katika Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo ataendelea  na Ziara hiyo katika Mkoa wa Kaskazini katika Shehia ya Donge na Nungwi ili kuangalia shughuli na miradi ya Chama cha Mapinduzi CCM.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.