Raia wa Denmark auwa mama na mwane wa miaka 4

Msanii wa Nigeria Zainab Ali-Nielsen maarufu kama Alizee na mtoto wake wa miaka minne wameuawa na mume wa msanii huyo ambaye ni raia wa Denmark, Peter Nielesen katika nyumba yao iliyoko huko Banana.

Polisi ya Nigeria imesema kwamba walipata taarifa kutoka kwa meneja wa eneo hilo Mr. Kunle Kukoyi, ambaye naye alipata taarifa kutoka kwa mdogo wa marehemu Gift Madaki kuwa alimsikia dada yake akilia kutokana na kupigwa na mumewe, na kisha hakusikia tena sauti, na ndipo walipoita polisi na kukuta mwanamuziki huyo akiwa na binti yake wa kike wakiwa wamelala chini, huku kukithibitishwa kifo chao kutoka kwa daktari.

Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa miili hiyo imekutwa na alama za vidole vya bwana Nielsen, na kwamba mauaji hayo yalijiri chumbani lakini miili yao iliburuzwa mpaka jikoni ambako ilifichwa.

Miili ya watu hao imehifadhiwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi, huku lebo iliyokuwa ikimsaidia msanii huyo ikitaka ubalozi wa Denmark kufanya uchunguzi maalum kujua nini hasa kilichojiri kwenye mauaji hayo.